Baraza La Wanawake Chadema (BAWACHA) limetangaza kufungua Kesi ya Kikatiba katika Mahakama Kuu ya Tanzania kuomba tafsiri ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 66 (1) kuhusu rais kuteua wabunge na kuwazuia walioteuliwa hivi karibuni kuapishwa.
Mpaka sasa Rais John Magufuli amekwisha teua wabunge nane ambapo kati yao wanawake ni wawili ambao ni Dk. Tulia Akson na Profesa Joyce Ndalichako huku wengine wanaosalia wakiwa ni wanaume.
Idadi hiyo ya wabunge nane waliokwisha kuteuliwa na rais inajumuisha uteuzi wa Januari 16, mwaka huu ambapo Profesa Palamagamba Kabudi na Alhaji Abdallah Bulembo waliteuliwa.
Akizungumza leo katika ofisi za Chadema Kanda ya Ziwa Victoria, Mwenyekiti wa Bawacha Taifa, Halima Mdee alisema kwa muda mrefu sasa toka kuingia utawala wa serikali hii ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli, kumekuwa na ukiukaji wa katiba.
Alisema awali ilianza kupigwa marufuku mikutano ya vyama vya siasa ambavyo vipo kwa mujibu wa Katiba ikiwa ni kumteua mmoja waliokuwa maofisa wa Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWT) kuwa mtendaji wa chama japo baadaye walilazimika kutangaza kastaafu jeshini.
“Katika katiba yetu ibara ya 66 (1)(e) rais anayo mamlaka ya kuteua wabunge wasiozidi kumi kutoka miongoni mwa watu wenye sifa zilizotajwa katika aya za (a) na (c) za Ibara ya 67 (1) na kati yao anapaswa kuteua angalau wanawake watano,” alisema.
Sign up here with your email