YONO YASIMAMIA MANJI KUONDOKA QUALITY PLAZA - Rhevan Media

YONO YASIMAMIA MANJI KUONDOKA QUALITY PLAZA

Tokeo la picha la Jengo la Quality Plaza
KAMPUNI ya Quality Group Ltd , inayomilikiwa na Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Yusuph Manji imeondolewa kwa nguvu kwa amri ya Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi, kwenye jengo iliyokuwa imepanga la Quality Plaza, baada ya kushindwa kulipa deni la Sh Bilioni 13, inayodaiwa na mmiliki wa jengo hilo, ambao ni Mfuko wa Pension wa PSPF.
Wakitekeleza kazi hiyo jana jijini Dar es Salaam, Kampuni ya Udalali ya Mahakama ya Yono waliopewa idhini na mfuko huo kuwatoa wadaiwa hao baada ya kushindwa kesi, kufuatia hukumu ya Mahakama Kuu iliyotolewa Novemba 24 mwaka huu, walitoa vyombo nje baada ya kupewa saa 24 kuondoa kwa hiari.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Yono, Scholastika Kevela ambao ndio watekelezaji wa kazi hiyo alisema, walitoa notisi ya saa 24 waliyoibandika juzi kwenye ofisi hiyo wakiwataka waondoke wenyewe kabla ya amri hiyo halali ya Mahakama haijaisha ifikapo leo asubuhi.
“Quality Group na wenzake wanne wanatakiwa kuondoka na sisi leo(jana) tumekuja kuwaondoa na ndio unaona wanapakia vitu vyao na kuondoka, wanadaiwa Dola Milioni 601 sawa na Sh Bilioni 13, ambazo kila mara akiambiwa alipe amekuwa akikimbilia mahakamani zaidi ya miaka 10 sasa”,alisema Kevela.
Alisema Mfuko wa PSPF,unaidai Kampuni ya Quality Group fedha hizo za upangaji, lakini kila anapotakiwa kulipa amekuwa akigoma na kukimbilia mahakamani kuweka pingamizi la kulipa ili aendelee kukaa bure na kwamba uamuzi wa Mahakama Kuu uliotolewa Novemba 24, umemtaka aondoke ndani ya saa 24 na kulipa deni analodaiwa.
“Tulikuja kubandika tangazo la hukumu hiyo la kumtaka aondoke mwenyewe kwenye jengo hilo lakini akawa anachana na watu wake na sisi tukaongeza watu wetu kulinda na sasa ameanza kutoa mali zake na hadi kesho anapaswa awe amemamliza,”alisema Kevela.
Alisema pamoja na kutoa vitu vyake ndani ya jengo hilo amepewa muda wa siku 14 kisheria awe amelipa deni hilo na kama atashindwa kulipa mali zake zitakamatwa na kuuzwa ili kupata fedha za kulipa deni analodaiwa na PSPF.
Kampuni nyingine zilizoamriwa kuondoka ndani ya jengo hilo ni Gaming Management Ltd, Q-cosult Ltd, International Transit Investiment ltd.
Previous
Next Post »