WAZIRI MUHONGO AIPONGEZA KAMPUNI YA ACACIA KWA KUWA KAMPUNI YA KWANZA YA MADINI KUWA NA HATI FUNGANI - Rhevan Media

WAZIRI MUHONGO AIPONGEZA KAMPUNI YA ACACIA KWA KUWA KAMPUNI YA KWANZA YA MADINI KUWA NA HATI FUNGANI

muhogo
“Nimetaarifiwa kwamba Acacia ndio kampuni ya kwanza ya uchimbaji
madini kutekeleza kipengele hiki cha sheria hii ya Madini ya mwaka 2010,
napenda niwapongeze sana kwa hatua mliyofikia yakutoa hakikisho la kukarabati
mazingira kwenye migodi yenu pindi mtakapositisha shughuli za uchimbaji.”
Alisema Profesa Muhongo, mara baada ya kusaini mkataba huo.
Kwa mujibu wa Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Migodi nchini, (Acting Chief
Inspector of Mine), Mhandisi Noel Baraka, alisema, nijukumu la kisheria kwa migodi
yote nchini, ya kati na mikubwa kuandaa mpango wa kufunga mgodi ambao shughuli
hiyo inasimamiwa na kamati ya kitaifa ya kusimamia shughuli za ufungaji migodi
(National Mine Closure Committee).
Kamati hiyo inaundwa na wawakilishi kutoka Wizara ya Nishatina
Madini, Ofisi ya Makamu wa Rais, Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira,
(NEMC), Wizara ya Maliasili na Utalii , Wizara ya Maji na Umwagiliaji, National
Land Use Planning Commission, viongozi wa Serikali ya mkoa na Wilaya ulipo
mgodi husika.
Mhandisi Baraka alifafanua kuwa Kampuni ya Acacia, iliandaa
mipango ya ukarabati wa mazingira pindi shughuli za uchimbaji zitakaposimama na
gharama zinazohusiana na ukarabati huo wamigodi yake mitatu ya Bulyanhulu,
Buzwagi na North Mara.
“Mpango huo na gharama zake ulipitiwa na kamati ya kitaifa ya
ufungaji migodi na kuridhishwa na baada ya kuridhishwa ulipitishwa ambapo leo
ni hatua ya mwisho ambapo Waziri wa Nishati na Madini, kwaniaba ya Serikali na
kiongozi wa Acacia, kwaniaba ya makampuni tanzu wanatia saini mkataba huo.”
Alisema Mhandisi Baraka na  kuongeza,
“Chini yamkatabahuu, dhamana (bonds) ya gharama za ukarabati kwa
mgodi wa Bulyanhulu, ni Dolaza Kimarekani 3,287,714, Mgodiwa North Mara ni Dola
za Kimarekani 19,164,344 na Mgodi wa Buzwagi ni Dola za Kimarekani 18.628,489.”
Alifafanua
“Sheria hii, kampu ni ya uchimbaji madini inapaswa kuweka hati
fungani (rehabilitation bonds) kwenye kampuni ya bima au benki, ili shughuli za
uchimbahji zinapo koma kwa sababu yoyote ile, basi fedha hizo ziweze kutumika kukarabati
mazingira ya eneo la shughuli ya uchimbaji nakuyarejesha katika hali bora na
salama.” Alisisitiza.
Kwaupande wake, Mshauri Mkuu wa Mazingira wa Kampuni ya Acacia,
Bi. Rebecca Stephen, alisema kampuni yake imefurahi sana kufikia hatua hiyo ya
kusaini mkataba huo, kwani  ni hakikisho kwamba fedha tayari zimetengwa
kwaajili ya shughuli hiyo.
“Kazi hii ilikuwa na mchakato mrefu uliochukua takribani
miaka miwili, na ulianza kwa kuandaa mpango wa ufungaji mgodi na gharama zake,
na kupitiwa na Wizara na kamati nzima na kupitishwa.” Alisema
Alisema Kampuni ya Acacia katika utekelezaji wa shughuli zake,
inazingatia siku zote kutii sheria za nchi na tukio la leo nimoja ya vielelezo,
alisema Bi. Rebeca.
“Sheriayamadini ya 2010 inahitaji kuwepo na hakikisho kutoka kwetu
ya namna gani tutakarabati mazingira pindi shughuli za uchimbaji zitakaposimama
na kuhakikisha pesa za kufanya ukarabati huo zipo,”  alisema na kuongeza
Acacia imetekeleza hiyo sheria tukiwa ndio kampuni ya kwanza kufikia hatua hii,
alisema Bi. Rebecca.
Normal
0

false
false
false

EN-US
X-NONE
X-NONE

MicrosoftInternetExplorer4

Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, (kulia), na Makamu wa Rais wa
Kampuni ya uchimbaji madini, Acacia (anayeshughulikia kampuni), Bw. Deo
Mwanyika, wakibadilishana hati baada ya kusaini mkataba wa hati fungani makao
makuuya Wizara hiyo jijini Dar es Salaam, hivi karibuni. Acacia imekuwa kampuni
ya kwanza ya uchimbaji madini nchini, kutekeleza sheria ya madini ya mwaka 2010
inayotaka kila kampuni kuwasilisha mpango wake wa ukarabati wa mzingira na
kuweka bond fedha pindi shughuli za uchimbaji zinapokoma. Wanaoshuhudia ni
wanasheria wa Wizara na kampuni ya Acacia

/* Style Definitions */
table.MsoNormalTable
{mso-style-name:”Table Normal”;
mso-tstyle-rowband-size:0;
mso-tstyle-colband-size:0;
mso-style-noshow:yes;
mso-style-priority:99;
mso-style-qformat:yes;
mso-style-parent:””;
mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;
mso-para-margin-top:0in;
mso-para-margin-right:0in;
mso-para-margin-bottom:10.0pt;
mso-para-margin-left:0in;
line-height:115%;
mso-pagination:widow-orphan;
font-size:11.0pt;
font-family:”Calibri”,”sans-serif”;
mso-ascii-font-family:Calibri;
mso-ascii-theme-font:minor-latin;
mso-fareast-font-family:”Times New Roman”;
mso-fareast-theme-font:minor-fareast;
mso-hansi-font-family:Calibri;
mso-hansi-theme-font:minor-latin;}


Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, (kulia), na Makamu wa Rais wa
Kampuni ya uchimbaji madini, Acacia (anayeshughulikia kampuni), Bw. DFeo
Mwanyika, wakitia saini mkataba wa hati fungani makao makuuya Wizara hiyo
jijini Dar es Salaam, hivi karibuni. Acacia imekuwa kampuni ya kwanza ya
uchimbaji madini nchini, kutekeleza sheria ya madini ya mwaka 2010 inayotaka
kila kampuni kuwasilisha mpango wake wa ukarabati mzingira na kuweka bondi
fedha pindi shughuli za uchimbaji zinapokoma.

 Profesac Muhongo, (kulia), akimsikiliza Bw. Mwanyika mwanzoni mwa hafla hiyo ya kutia saini, mkataba wa hati fungani
 Waziri Muhongo (kushoto), akizungumza mwanzoni mwa hafla hiyo
Makamu wa Rais wa Acacia, Bw. Deo Mwanyika, (kulia) na
Mshauri Mkuu wa Mazingira wa kampuni hiyo, Bi. Rebeca Stephene,
wakipitia nyaraka hizo kabla ya kusaini
Makamu wa Rais wa Acacia, Bw. Deo Mwanyika, (kulia) na Mshauri Mkuu wa Mazingira wa kampuni hiyo, Bi. Rebeca Stephene, wakipitia nyaraka hizo kabla ya kusaini
  Waziri Muhongo (kulia), akizungumza mwanzoni mwa hafla hiyo
 Waziri Profesa Muhongo, akitia saini mkataba huo wa hati fungani
Makamu wa Rais wa Acacia, Bw. Deo Mwanyika akitia saini mkataba huo wa hati fungani
Previous
Next Post »