Urusi imeyahusisha mauaji ya Balozi Andrey Karlov na tukio la kigaidi.
Balozi huyo alipigwa risasi na mshambuliaji aliyekuwa akipaza sauti akitaja AleppoMsemaji wa wizara ya mambo ya kigeni mjini Moscow amesema Uturuki wamehakikishiwa kwamba kutakuwa na uchunguzi wa kina kuhusiana na tukio hilo na wote watakaokuwa wamehusika wataadhibiwa.
Meya wa Ankara amesema mauwaji hayo yamelenga huharibu mahusiano ya nchi hiyo na Urusi. Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani John Kerry amesema Marekani iko tayari kusaidia katika uchunguzi wa tukio hilo.
Sign up here with your email