WANAFUNZI WA IBUN JAZARY ISLAMIC WAPONGEZWA KWA KUFANYA VIZURI KWENYE MTIHANI WAO. - Rhevan Media

WANAFUNZI WA IBUN JAZARY ISLAMIC WAPONGEZWA KWA KUFANYA VIZURI KWENYE MTIHANI WAO.



Shule ya Ibun Jazary Academic primary School imefanya mahafali ya tano jana  hii katika ukumbi wa karimjee Hall jijini Dar es salaam ili kuwapongeza vijana wao waliohitimu darasa la Saba na kufanya vizuri katika matokeo yao.

Akizungmza na wanafunzi wakati wa  mahafali hayo Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Baraza la Waislamu Bakwata Sheikh Hamis Mataka kwa niaba ya Mufti kuu wa Tanzania amesema tunawapongeza wanafunzi hawa kwa matokeo mazuri waliyoyapata na kuweza kufanya vizuri kwenye elimu ya elimu paomoja  na dini.

"watoto wengi huwa wanaosoma shule hizi za dini wanakuwa wanazingatia elimu ya dini lakini watoto hawa wamejibu changamoto kwa kufanya vizuri katika vyote yani katika elimu ya dini na elimu ya dunia hivyo nawapongea sana,"amesema Mataka

Hivyo hivyo mkuu wa shule hiyo Othuman Kaporo amewapongeza waanafunzi hayo kwa kumaliza darasa la saba nakuongeza kuwa wanafunzi wote wanaomaliza katika shule yake ni desturi yao kufanya vizuri katika wilaya,Mkoa na kitaifa kwenye mitihani yao.

Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Bakwata,Sheikh Khamis Mataka akizungumza katika mahafali ya Shule ya Ibun Jazary Academic Primary School katika kitika ukumbi wa karimjee Hall jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi wa Tasisi za Mkuu wa shule hiyo Ibun Jazary Othman Kaporo akizungumza katika mahafali ya Shule ya Ibun Jazary Academic Primary School katika ukumbi wa karimjee Hall jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Bakwata,Sheikh Khamis Mataka akimkabidhi tuzo mwanafundi aliefanya vizuli,Ghukba Kassim Rashid jana katika ukumbi wa karimjee Hall jijini Dar es salaam.




Wageni mbalimbali pamoja na wazazi wakimsikiliza Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Bakwata,Sheikh Khamis Mataka

Previous
Next Post »