Serikali
imepiga marufuku kuagiza na kuingiza nyama za kuku waliochinjwa kutoka
nje ya nchi ili kulinda afya za walaji wa bidhaa hiyo ya nyama nchini.
Katazo
hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mhe. William
Tate Ole Nasha kwenye mahojiano maalum na EATV ilipotaka kupata
ufafanuzi wa serikali kuwa inahakikisha vipi nyama na vitoweo kutoka nje
ya nchi zinaingizwa nchini zikiwa na ubora unaokidhi viwango vya afya
kwa walaji.
Ole
Nasha amesema hairuhusiwi kuagiza wala kuuza kuku waliochinjwa kutoka
nje ya nchi kwakuwa kwa sasa nchi inajitosheleza na inajitegemea kwa
kiwango kikubwa cha nyama.
Amewataka
wafugaji na wafanyabiashara kutumia fursa za kuzalisha nyama kwa tija
na ubora zaidi ili nchi ianze kuuza vitoweo vya nyama hasa kuku nje ya
nchi.
Ameongeza
kuwa tayari serikali inaendelea kuchukua hatua za kisheria kwa viongozi
wanaoshirikiana na wafanyabiashara wasio waaminifu kuingiza nyama hizo
za kuku wa nje nchini.
Sign up here with your email