Rais Mteule wa Gambia amekuwa akiongea juu ya anavyotazamia kubadilisha taifa tangu ashinde bila kutarajia juma lililopita.
Adama
Barrow, ambaye alikuwa akifanya kazi kama mfanyabiashara wa kujenga
nyumba na kuuza, alimshinda Yahya Jammeh, aliyenyakua madaraka kwa mtutu
wa bunduki na kutawala kwa miaka 22.Makundi ya haki za binadamu yamemlaumu Bw Jammeh kwa ukiukaji wa haki za watu wa mapenzi ya jinsia moja, waandishi wa habari na wanasiasa wa upinzani.
- Upinzani ''wapata ushindi wa mapema'' Gambia
- Wasifu wa rais mteule wa Gambia Adama Barrow
- Kiongozi wa upinzani ashinda uchaguzi wa urais Gambia
Bwana Barrow aliambia shirika la habari la Associated Press kuwa atawaachilia kutoka gerezani wanasiasa wote wa upinzani walio gerezani.
Yeye pia alisisitiza kuwa atabadili msimamo wa awali wa Bw Jammeh wa kutaka kuondoa Gambia katika mahakama ya Kimataifa ya uhalifu wa kivita, ICC, na Jumuiya ya Madola.
Raia wengi wa Gambia walikesha usiku wote wakisherehekea kuondoka kwa Bw Jammeh, ambaye amesema kuwa ataendelea na shughuli zake za kilimo.
Lakini changamoto nyingi zipo.
Taifa hilo ni maskini sana, na wananchi wengi wachanga wametorokea mataifa ya ng'ambo.
Sign up here with your email