MZEE WA UMRI 101 AHUKUMIWA JELA MIAKA 13 KWA KOSA LA UBAKAJI - Rhevan Media

MZEE WA UMRI 101 AHUKUMIWA JELA MIAKA 13 KWA KOSA LA UBAKAJI

ralph-clarke
Mzee mwenye umri wa miaka 101 amehukumiwa kwenda jela kwa miaka 13 kwa makosa ya ubakaji na kujihusisha na mapenzi na wasichana wenye umri mdogo na alitenda makosa hayo kati ya 1970 na 1980.
 Mzee dereva mstaafu wa malori makubwa, Ralph Clarke aliwahi kupewa onyo kali juu ya kuweza kuhukumiwa kifungo cha kutumikia jela kwa makosa 17 kama hayo, na mmoja ya makosa yake makubwa ni kufanya mapenzi na mtoto mdogo na jaribio la kujeruhi kimapenzi kwa kutaka mapenzi kwa watoto kwa kutumia nguvu.
Clarke, anaaaminika kwamba ni mmoja wa watu wenye umri mkubwa kabisa kuweza kushtakiwa na kisha kuhukumiwa kwenda jela kwa makosa ya ubakaji katika historia ya Uingereza.
Alikutwa na makosa tisa kati ya 17 baada ya mahakama mjini Birmingham kumtia hatiani na kumpa adhabu hiyo ya miaka 13 jela.
Previous
Next Post »