Mwanamuziki Mwasiti ambaye
anafanya vizuri na wimbo wake 'Kaa nao' amefunguka na kuweka hadharani
sifa za mwanaume ambaye anahitaji kuwa naye katika maisha yake na kusema
haiwezekani hata siku moja mtu na mpenzi wake wakawasiliana mara moja
kwa siku
Mwasiti akiwa katika kipindi cha Planet Bongo
Akiongea
kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, Mwasiti amesema
kuwa angependa mume wake kwanza awe mcha Mungu na mwelewa ili wapendane
na kujaliana kweli ila yote hayo yabebwe na msingi mkuu wa mapenzi ambao
ni mawasiliano mazuri kati yao.
"Mwanaume wangu mimi awe anampenda sana Mungu kwani mimi naheshimu sana dini yangu, hivyo napenda mume wangu awe mcha Mungu mwelewaji, understanding, caring, loving and sharing hivi vinne ndiyo muhimu. Tupendane, tugawane, tuelewane na tufanye mawasiliano kwa sababu wewe huwezi kuwa boyfriend harafu siku nzima usiku tu ndiyo unatoka na ujumbe wa simu eti 'good night' hata kama mtu yupo busy lakini hakuna ubusy wa namna hiyo kwa waubani" alisema Mwasiti

Sign up here with your email