Polisi nchini
Argentina wamepambana na waandamanaji walio kuwa wakijaribu kuingia
katika mahakama moja alipofikishwa mwanaharakati maarufu Milagro Sala,
anayetuhumiwa kwa Rushwa, ambapo Polisi,raia wamejeruhiwa katika
makabiliano hayo.
Baadhi ya wabunge wa upinzani wana walaumu polisi kwa vitendo vya kikatili. Mwanaharakati huyo, Milagro Sala ni mwenyeji wa Argentina na ni mwenyekiti wa kikundi kijulikanacho kama Tupac Amaru social welfare group, kinachosambaza misaada ya kijamii kwa wananchi wanaoishi katika mazingira magumu kusini mwa jimbo la Jujul nchini humo.
Mwanaharakati huyo amesema anatuhumiwa na mamlaka za serikali kutokana na kuwa na maoni yenye mtazamo tofauti na serikali inavyotaka.
Sign up here with your email