WATOTO
yatima wa kituo cha Daily Bread Life Ministres cha Mkimbizi katika
Manispa ya Iringa na wale wa kituo cha Tosamaganga katika wilaya ya
Iringa Iringa wapewa msaada wenye nguo na chakula msaada wenye thamamani
ya Tsh milioni 3 kwa ajili ya sikukuu ya Chrismas na mwaka mpya .
pamoja
na msaada huo wa chakula na mavazi pia Mungai aliahidi kuchangia Tsh
milioni 1.5 kwa ajili ya ununuzi wa vyombo vya muziki katika kituo hicho
na kufanya msaada wake kufikia Tsh milioni 4.5
Huku
mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela pamoja na kumshukuru
mfanyabiashara huyo kwa kukumbuka yatima bado ametoa onyo kali kwa
wanawake wote wanaotupa watoto kuwa ikibainika watachukuliwa hatua kali .
Akizungumza
baada ya kukabidhi msaada huo Geofrey Mungai alisema imekuwa ni kawaida
ya familia yake kila mwaka kusherekea sikukuu mbali mbali pamoja na
watoto yatima kama sehemu ya kuikumbusha jamii kuwa na utamaduni wa
kuwatazama yatima hao ambao tegemeo lao kubwa ni jamii inayowazunguka.
Mungai
alisema kuwa suala la kulea yatima linapaswa kuwa ni jukumu la
watanzania wote na kuwa ili kuwawezesha watoto hao kujisikia ni sehemu
ya familia zenye wazazi ni vema jitihada za vituo vya yatima hapa nchini
kuendelea kuheshimika zaidi.
Hata
hivyo Bw.Mungai alisifu kazi nzuri inayofanywa na kituo hicho cha DBL
katika kuendelea kuwalea watoto ha kimwili na kiroho na kuendelea kuwa
miongoni mwa vituo bora vya kulea yatima katika mkoa wa Iringa.
Aidha
aliwataka wananchi wengine kuendelea kufika katika kituo hicho na
kusaidia kulea watoto hao kwa kutoa misaada mbali mbali kama njia ya
kuwafariji na kuwalea watoto hao kuliko kuwaachia walezi wao pekee.
Hivyo
alisema kwa mwaka huu amelazimika kutoa msaada wa nguo na chakula kwa
kila kituo msaada wenye thamani ya Tsh milioni 1.5 na kuwa ataendelea
kufanya hivyo kwa ajili ya watoto hao ili siku ya sikukuu nao waweze
kufafana na watoto wengine ambao wanawazazi wao wote wawili .
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela (kushoto ) na mfanyabiashara Geofrey Mungai wakiwa wamewapakata watoto yatima wa kituo cha Daily Bread Life Ministres cha Mkimbizi katika Manispa ya Iringa waliokuwa wametupwa na wazazi wao na kuchukuliwa na kituo hicho jana wakati Mungai alipofika kukabidhi chakula na nguo za sikukuu ya Krismas na mwaka mpya kwa watoto hao
Mkuu wa wilaya ya Iringa Bw Kasesela akisalimiana na Geofrey Mungai kulia
Viongozi mbali mbali wakiwa katika picha ya pamoja na yatima wa kituo cha DBL kutoka kushoto ni mkurugenzi wa kituo hicho mchungaji Mpeli Mwaisumbe , mfadhili Geofrey Mungai , katibu wa CCM Iringa , mwenyekiti wa CCM Iringa mjini , mkuu wa wilaya ya Iringa Bw kasesela,mbunge viti maalum Iringa Ritta kabati ,diwani Dolla Nziku
Sign up here with your email