MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFUNGUA MKUTANO WA WADAU WA KUENDELEZA MAENEO TENGEFU YA VIWANDA VYA USINDIKAJI VYAKULA - Rhevan Media

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFUNGUA MKUTANO WA WADAU WA KUENDELEZA MAENEO TENGEFU YA VIWANDA VYA USINDIKAJI VYAKULA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ipo mbioni kupunguza muda wa utoaji wa leseni za biashara nchini ili kutoa fursa kwa wananchi wengi zaidi kupata leseni hizo kwa ajili ya shughuli za kibiashara.


Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wakati anafungua mkutano wa wadau wa kuendeleza maeneo tengefu ya viwanda vya usindikaji wa vyakula nchini.


Makamu wa Rais amesema mpango utaenda pamoja na kupunguza baadhi ya kodi na tozo ambazo ni kero kwa wananchi hasa wenye viwanda kama hatua ya kukuza biashara na uwekezaji katika sekta ya viwanda nchini.


Amesisitiza kuwa Serikali inaendelea na mazungumzo na wenye mabenki hususani benki ya TIB ili kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa wawekezaji wenye nia ya  kuanzisha viwanda.


Kuhusu usindikaji wa bidhaa nchini, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mjumbe katika jopo la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa la kumuwezesha mwanamke kiuchumi akiwakilisha nchi za ukanda wa Kusini na Mashariki mwa Afrika amepongeza jitihada zinazofanywa na wasindikaji wadogo nchini katika utengenezaji wa bidhaa mbalimbali ambazo zitakidhi katika masoko ya ndani na nje ya nchi.


“Serikali inafarijika sana kuona kuwa wasindikaji wadogo nchini wamethubutu na wana uwezo wa ushindani katika biashara ya ndani na hata nje, hivyo tunayohaki ya kujigamba kwa kuthubutu, Tumeweza na Tuendelea Kusonga mbele



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema umefika wakati kwa Wizara na taasisi za Serikali na wadau wa maendeleo kuona umuhimu wa kuhakikisha viwanda vinajengwa vijijini ili mkulima mdogo anapolima awe na uhakika wa kupata soko katika viwanda hivyo.


Amesema kuwa hali hiyo itaondoa changamoto ya kusafirisha bidhaa nyingi ambazo zinaharibika njiani au zinapofika sokoni na hivyo kukosesha jamii kipato kilichotarajiwa.

Makamu wa Rais pia amehimiza watafiti nchini wajielekeza katika kufanya tafiti ambazo zitasaidia sekta binafsi na serikali kwa ujumla kuhusu namna bora ya kukuza sekta ya viwanda nchini.

Kwa upande wake, Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage amekiri kuwa bado kuna changamoto kubwa ya maeneo ya yatakayojengwa  viwanda na kwamba Serikali imeliona tatizo hilo na inalifanyia kazi ambapo tayari  imeshaziagiza Halmashauri zote nchini kujenga maeneo kwa ajili ya viwanda.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati ufunguzi wa mkutano wa Wadau wa kuendeleza maeneo Tengefu ya Viwanda vya Usindikaji Vyakula uliofanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati ufunguzi wa mkutano wa Wadau wa kuendeleza maeneo Tengefu ya Viwanda vya Usindikaji Vyakula uliofanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam ambapo aliwapongeza TAPOFA kwa kazi nzuri wanayoifanya lakini pia aliwataka Wasindikaji kuongeza ushirikiano ili kufikia maendeleo na mafanikio ya juu.
Wadau waliohudhuria na kushiriki wakimsikiliza kwa makini Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati ufunguzi wa mkutano wa Wadau wa kuendeleza maeneo Tengefu ya Viwanda vya Usindikaji Vyakula uliofanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa TAFOPA Bi. Suzy Laizer akihutubia wakati ufunguzi wa mkutano wa Wadau wa kuendeleza maeneo Tengefu ya Viwanda vya Usindikaji Vyakula uliofanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, mgeni rasmi kwenye mkutano huu alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia bidhaa mbalimbali za vyakula vilivyosindikwa zinazotengenezwa na wajasiriamali   muda mfupi kabla ya kufungua wa mkutano wa Wadau wa kuendeleza maeneo Tengefu ya Viwanda vya Usindikaji Vyakula uliofanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Previous
Next Post »