Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Munngano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akihutubia kwenye Uzinduzi wa Bodi ya Udhamini dhidi ya Ukimwi
uliofanyika tarehe 1 Desemba kwenye hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es
Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Munngano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akikata utepe katika vitendea kazi kama ishara ya Uzinduzi wa Bodi ya Udhamini dhidi ya Ukimwi
uliofanyika tarehe 1 Desemba kwenye hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es
Salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Munngano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akionyesha vitendea kazi atakavyovikabidhi kwa bodi mara baadaya ya kuizindua Bodi ya Udhamini dhidi ya Ukimwi
uliofanyika tarehe 1 Desemba kwenye hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es
Salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Munngano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini dhidi ya Ukimwi Bw.
Godfrey Simbeye vitendea kazi vya bodi hiyo mpya katika hafla ya
uzinduzi wa bodi hiyo
uliofanyika tarehe 1 desemba kwenye hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es
Salaam.
...................................................................................................
...................................................................................................
Makamu
wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amezindua Bodi ya Udhamini dhidi ya UKIMWI na
kuwagawia vitendea kazi sambamba na uzinduzi wa mpango wa hiari wa familia
kuchangia mfuko wa UKIMWI, shughuli iliyokwenda sambamba na maadhimisho ya siku
ya Ukimwi duniani ambayo huadhimishwa duniani kote desemba mosi.
Madhumuni
ya Bodi hiyo ni kujenga nguvu ya ndani ya kifedha pamoja na kuhakikisha uwepo
wa rasilimali za kutosha katika kupambana na ugonjwa wa Ukimwi ambao bado ni
tishio huku tafiti za mwaka 2015 zikionesha kuwa takribani watu 48,000
huambukizwa VVU kila mwaka nchini, huku watu milioni 1.5 wakiishi na VVU kati
yao wastani wa laki nane wanatumia dawa za kufubaza
virusi vinavyosababisha UKIMWI.
Akizungumza
katika uzinduzi huo, Makamu wa Rais amesema kazi kubwa ya kutafuta kutunisha
mfuko itakuwa ni chachu katika kupambana na ugonjwa huo na kuitaka bodi hiyo
kubuni mbinu za kutunisha mfuko huo kufuatia ukweli kwamba uhisani una mwisho
na uhisani una vipaumbele vyake kutokana na wakati husika.
Katika
harambee iliyofanyika jana usiku wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo,zaidi ya milioni 340 zilipatikana.
Sign up here with your email