MAGARI YA DISEL KUPIGWA MARUFUKU MIJI KADHAA ULAYA - Rhevan Media

MAGARI YA DISEL KUPIGWA MARUFUKU MIJI KADHAA ULAYA

  • Magari yanayotumia Diesel kupigwa marufuku katika miji kadhaa Ulaya
     
Magari yanayotumia Diesel kupigwa marufuku katika miji kadhaa Ulaya
Mameya kutoka miji minne mikubwa duniani wamesema watapiga marufuku magari na malori yanayotumia mafuta ya Diesel katika miji yao ifikapo mwaka 2025.
Viongozi hao kutoka miji ya Paris, Mexico City, Madrid na Athens wamesema wanataka kuhakikisha kuwepo na hewa safi.
Shirika la Afya duniani{WHO} linakadiria kwamba watu milioni tatu hufariki kila mwaka kutokana na hewa chafu duniani.
Azimio la mameya hao liliafikiwa kwenye kongamano la kimataifa nchini Mexico.
Wataalamu wa afya wanasema moshi unaotoka kwa magari yanayotumia Diesel huingia kwa mapafu ya binadamu na kusababisha ugonjwa na kupumua na moyo.
Mameya hao wamesema wataweka magari m'badala yanayotumia umeme, na kawi ya maji.
Previous
Next Post »