Kesi
iliyokuwa isikilizwe 21 Disemba 2016 inayomkabili Mbunge wa Arusha
Mjini, Godbless Lema pamoja na mkewe, Neema Lema wakituhumiwa kumtukana
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo imeahirishwa kutokana na hali ya
Godbless Lema kuwa mbaya gerezani.
Taarifa
za Godbless Lema kushindwa kufika mahakamani zimetolewa na wakili wa
serikali Elizabeth Swai kwa Hakimu Mfawidhi katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi, Augustino Rwezile ambapo alisema kuwa alipata taarifa kutoka kwa
Afisa Magereza zikieleza kuwa mbunge huyo anaumwa na amepewa mapumziko
hivyo asingeweza kufika mahakamani.
Aidha, taarifa kutoka kwa kiongozi huyo wa magereza hazikueleza wazi kuwa mbunge huyo anaugua ugonjwa gani.
Kuhusu
kesi hiyo inayowakabili wanandoa hao wawili jana walikuwa wasomewe
hoja za awali ambapo pia shahidi wa kwanza kutoka upande wa Jamhuri,
George Katabazi alikuwa atoe ushahidi.
Godbless
Lema na Neema Lema wanakabiliwa na kesi ya kumtukana Mkuu wa Mkoa wa
Arusha kitendo wananchodaiwa kuwa walikitenda kupitia ujumbe mfupi wa
simu mara baada ya Rais Magufuli kumteua Mrisho Gambo kuuongoza mkoa
huo.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe 18 Januari 2017.
Sign up here with your email