KESI ya kupinga kuendelea kwa uongozi wa askofu Jackob Mameo Ole Paulo wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki imeahirishwa hadi tarehe 19 Januari mwakani,
Erick Rwehumbiza, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro alilazimika kuahirisha kesi hiyo jana mahakamani hapo ili kupisha ushahidi wa kesi hiyo utakaoanza kutolewa 19 Januari 2017.Akisoma maelezo ya shauri hilo Hakimu Rwehumbiza amesema kesi hiyo ilifikishwa mahakamani baada ya uchaguzi wa kura za imani wa kanisa hilo kukamilika hapo tarehe 25 Juni, 2015 na kuonekana kuwa na kasoro.
Katika kesi hiyo mlalamikaji ni Robert Mwanga ambaye pia alikuwa mgombea mwenza wa kiti hicho na kushindwa, anadai kuwa Askofu Mameo anaendelea kuongoza baada ya kusimikwa bila ya kupata kura zinazofikia theluthi mbili kama Katiba ya kanisa lao inavyotaka.
Kwa mujibu wa mlalamikaji, kwa kura alizopata Askofu Mameo hakustahili kushinda na kwamba kumtangaza mshindi ni kukiuka Katiba ilihali uchaguzi huo ulipaswa kurudiwa.
Mbali na askofu huyo, washitakiwa wengine ni Tume ya Uchaguzi ya Kanisa na Bodi ya Usajili ya Kanisa hilo. Ezra Mwaluka ndiye wakili wa Askofu Mameo wakati Mariam Kapama ni wakili wa mlalamikaji.
Hakimu Rwehumbiza amesema, kesi hiyo itaendelea kusikilizwa kwa mashahidi wawili wa upande wa mlalamikaji kutoa ushahidi wao kwa siku mbili mfululizo huku wakifuatia mashahidi wa mshitakiwa.
Sign up here with your email