Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa RAHCO, Ndg Masanja Kadogosa leo amekutana na
wafanyabiashara waliovamia maeneo mbali mbali ya reli mkoani Dodoma na
kufanya mazungumzo nao. Wafanyabiashara hao wapatao 200 kutoka maeneo ya
stendi ya mkoa, na stend ya daladala ya Jamatini, walikusanyika katika
club ya reli (Dodoma railway club) kwa mazungumzo yaliyohusisha
changamoto mbali mbali wanazokutana nazo wakiwa katika maeneo hayo ya reli.
Mkurugenzi aliwahakikishia kuwa nia ya serikali sio kuwanyanyasa wafayabiashara hao au kuwapa usumbufu bali RAHCO kama kampuni inataka kuwabahini na kuwafahamu watu walipo katika maeneo ya reli na sio kwa mkoa wa Dodoma tu bali zoezi hili ni la nchi nzima maeneo ambayo reli inapita.
Sheria ya reli ya mwaka 2002 inaweka wazi juu ya maeneo ya reli (hifadhi ya reli),kuwa kwa maeneo ya mjini kutoka katika njia ya reli upande wa kushoto na kulia ni mita 15 na kwa maeneo ya vijijini ni mita 30,sheria hiyo inaendelea kusema kuwa mtu yeyote atakae fanya shughuli zake katika maeneo hayo ya reli bila kibali au makubaliano na RAHCO anakuwa amevunja sheria hiyo, hivyo kampuni hodhi ya
rasilimali za reli inaweza kumchukulia hatua mbali mbali ikiwemo kuvunja majengo au miundombinu iliyopo katika hifadhi hiyo. Mkurugenzi amewataka wafanyabiashara hao kupitia kwa viongozi wao waliopo kuanza kujiandaa kwa kuingia mkataba na RAHCO wa kufanya biaashara katika maeneo ya reli tofauti na hivi sasa ambapo wengine wanakaa bila kulipa kodi sehemu yoyote na wapo wanaolipa kodi kwa manispaa ya Dodoma wakati maeneo hayo ni ya RAHCO.
Kaimu Mkurugenzi wa RAHCO katikati, Bw.Masanja kadogosa akiongozana na baadhi ya viongozi wa wafanyabiashara katika maeneo ya reli wakielekea kukagua maeneo hayo ambapo wafanyabiahara hao wanafanya shuguli zao.
Mkurugenzi Kadogosa akiwasalimia wauza viatu waliopo katika eneo la reli nyuma ya stand ya daladala ya Jamatini wakati wa ukaguzi wa maeneo ambayo wafanyabiashara wengi wanalitumia.
Wafanyabiashara katika stendi ya Jamatini mkoani Dodoma, wakiendelea na shughuli zao wakati Mkurugenzi wa RAHCO Bwana Kadogosa akifanya ukaguzi katika maeneo ya reli yaliyopo hapa stand ya daladala ya Jamatini.
Sign up here with your email