Na: Sekela Mwasubila, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga Bwana Yusuf Semguruka ameahidi kuwawezesha wakazi wa kaya ya Milola kukamilisha ujenzi wa darasa moja katika shule ya Sekondari Ulanga.
Alitoa ahadi hiyo alipokuwa akijibu changamoto zilizojitokeza katika taarifa ya ujenzi wa madarasa matatu na ofisi mbili alipofanya ziara ya kujitolea nguvu kazi katika ujenzi huo ambapo aliongozana na kamati ya ulinzi na usalama.
Alisema kuwa Halmashauri iko pamoja na wananchi hao kwani imeweza kuwasaidia ujenzi wa madarasa matatu na haitashindwa kumalizia darasa moja ambalo wananchi wameamua kuliongeza ili kukabiliana na upungufu wa madarasa shuleni hapo.
Aliongeza kuwa wananchi hao waanze ujenzi huo na watakapofikia hatua nzuri wampe taarifa ili awawezeshe vifaa vya kumalizia darasa hilo na kuwaasa kuendeleza ushirikiano uliokuwepo toka ujenzi wa awali wa madarasa matatu kwani iwapo waligawana darasa moja kila kijiji kwasasa wajenge darasa hilo kwa umoja ili likamilike mapema.
Hata hivyo aliongeza kuwa ujenzi wa madarasa hayo ulichangiwa na watu mbalimbali ikiwemo kampuni ya uchimbaji wa madini ya Tanz Graphite ambao walijitolea mifuko 300 ya saruji, watumishi wa Halmashauri ambao walichangia milioni moja na laki nane hivyo wananchi wasikate tamaa kwani akikwama atawashirikisha wadau mbalimbali wa maendeleo ili kukamilisha darasa hilo.
Ziara ya kujitolea nguvu kazi katika ujenzi wa madarasa na ofisi mbili katika shule ya Sekondari Ulanga imefanyika shuleni hapo ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Mh. Joseph Kassema, Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya, Kamati ya Ulinzi na Usalama, wakuu wa Idara wa Halmashauri ya Wilaya na wananchi wa kata ya Milola na kuwezesha kumwaga zege katika vyumba viwili vya madarasa ujenzi ambao unafanywa na wananchi kujitolea nguvu kazi kwa kushirikia na diwani wa kata hiyo Mh. Msalam Mohamed Msalam.
Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Mh. Jacob Kassema akichanganya mchanga saruji na mchanga ikiwa ni kuwaunga mkono wananchi wa kata ya Milola katika ujenzi wa madarasa shule ya Sekondari Ulanga.
Afisa Usalama wa Wilaya ya Ulanga Bwana Paul Mtenjele (katikati) akimwaga kokoto kwenye mchanga tayari kwa ajili ya kuandaa zege la darasa katika shule ya Sekondari Ulanga.
Diwani wa kata ya Milola Mh. Msalam Mohamed Msalam akichanganya zege tayari.
Sign up here with your email