Golikipa mkogwe nchini Ivo
mapunda amesema uamuzi wake wa kuihama timu ya Tanzania Prisons
ulimfanya afungwe gerezani kwa madai ya kuliasi jeshi.
Golikipa Ivo Mapunda
Ivo amesema hayo wakati akisimulia safari yake ya soka nchini Tanzania, ambapo amesema alipokuwa akiidakia Prison alikuwa ni mtumishi wa Jeshi la Magereza kama askari Magereza lakini badaye wakati timu ya Moro United inaanzishwa, yeye na mwenzake Shadrack Nsajigwa waliitwa katika klabu hiyo.
Baada ya kusajiliwa klabuni hapo, walitakiwa kuondoka Prisons na kuacha kazi ya uaskari, jambo ambalo likuwa gumu kutokana na uongozi wa jeshi hilo mkoani Mbeya kuwawekea vikwazo kwa madai kuwa kuacha kazi ya jeshi ni sawa na kuliasi jeshi.
Ivo anasema katika mvutano huo, jeshi hilo liliamua kuwafunga gerezani kwa muda kama adhabu na pia wasipate nafasi ya kwenda Moro United, lakini baadaye waliachiwa na kuhamia Moro United, kabla ya kujiunga na Yanga.
Ivo amewahi kuvidakia vilabu vya Tanzania Prisons, Moro United, Yanga SC, St. George ya Ethiopia, African Lyon, Gor Mahia, Simba SC pamoja na timu ya Taifa ya Tanzania "Taifa Stars" na ameweka wazi kuwa timu anayoikubali Tanzania majimaji ya Songea, kwa kuwa hiyo ndiyo timu yake ya nyumbani.
N
Sign up here with your email