Wizara ya mashauri ya nchi za nje ya Uchina, inasema kuwa imepeleka malalamiko kwa upande unaohusika wa Marekani, baada ya Rais mteule Donald Trump, kuzungumza kwa simu na rais wa Taiwan.
Uchina inaona Taiwan kuwa ni jimbo lake lilojitenga.
Msemaji wa wizara alisema, Uchina ni moja, na ndio msingi wa kisiasa katika uhusiano baina ya Marekani na Uchina.
Mazungumzo ya simu baina ya Bwana Trump na Rais wa Taiwan, Tsai Ing-wen, yamevunja msimamo wa kidiplomasia kwa Marekani.
Hapo awali, waziri wa mambo ya nchi za nje wa Uchina, Wang Yi, alisema mazungumzo hayo ya simu ni "ujanja wa Taiwan usiokuwa na maana".Mwandishi wa BBC anasema ikiwa simu hiyo ni ishara ya mabadiliko ya sera za Marekani kuhusu Taiwan, basi Uchina itajibu kwa hasira.
Sign up here with your email