CHINA KUTENGENEZA MELI INAYOFANANA NA TITANIC - Rhevan Media

CHINA KUTENGENEZA MELI INAYOFANANA NA TITANIC

mfano wa mashua ya Titanic
Mashua sawia na iliyotengenezwa katika mji mkuu wa Belfast huko Ireland ya Titanic itawekwa katika eneo la kumbukumbu la theme park nchini India.
Ujenzi huo wa mashua hiyo yenye urefu wa kina cha mita 269, itawekwa katika hifadhi iliyoko mashambani , katika mkoa wa Sichuan, .
Ujenzi huo uliaza siku ya Alhamisi.
Mashua ya Titanic iliyojengwa na Harland na Wolff huko Belfast , iligonga mwamba wa barafu na kuzama Kaskazini mwa Atlantic mwaka 1912 hatua iliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 1,500.
Mashua hiyo ilikuwa katika safari yake kutoka Southampton ikielekea New York.
Habari kuhusu meli hiyo ni swala ambalo liliwashangaza raia wengi kutoka China.
Titanic
Hisia zaidi ziliibuka mwaka 1997, baada ya filamu iliyokuwa ikimuangazia Kate Winslet na Leonardo DiCaprio, kuwa maarufu nchini humo.
Titanic
Muelekezi wa filamu, James Cameron, kutoka Canada, alikuwa na mashua kama hiyo iliotengezwa kwa maswala ya uigizaji pekee , lakini hakuna mashua sawia na hiyo iliowahi kutengenezwa.
Bilionea mmoja kutoka Australia, Clive Palmer, alitangaza mipango yake ya kutengeneza mashua kama ya Titanic mwaka 2012, lakini mradi huo bado haujakamilika.
Meli hiyo ya China, itakuwa yenye umbo sawa na ile ya Titanic , itakuwa na sehemu ya michezo, maonyesho, kuogelea na sehemu maalum ya watu maalum ambayo itakuwa na mtandao wa Wifi na inatarajiwa kuwa kivutio kikubwa katika eneo hilo la theme park lililoko kilomita kadhaa kutoka pwani ya China.
Kampuni hiyo ilitangaza mipango wa mradi huyo, utakaogharimu Yuan bilioni moja mwaka 2014, kulingana na shirika la habari la AFP
Utalii wa ndani nchini China umeimarika kwa kiwango kikubwa, kupitia usaidizi wa serikali.meli ya Titanic
Previous
Next Post »