Maafisa
Usalama wa Rais mteule wa Marekani, Donald Trump wamemtembelea mtu
mmoja aliyetishia kumuua kiongozi huyo kwa ujumbe alioweka kwenye
mitandao ya kijamii.
Vyanzo
vya vyombo vya dola viliuambia mtandao wa TMZ kuwa kikosi maalum cha
mashushu wa usalama cha Trump pamoja na Mkuu wa Polisi msaidizi wa Ohio,
Jumatatu ya wiki hii walifika nyumbani kwa mtuhumiwa huyo aliyeweka
ujumbe wake kwenye mitandao Novemba 14 mwaka huu, ukisioma “Kill Trump”
(Muue Trump).
Ilielezwa
kuwa kikao kati ya maafisa hao wa usalama nyumbani kwa mtu huyo
anayetumia jina la ‘Micah’, kilienda vizuri ambapo aliwaeleza kuwa
alikuwa anatania tu huku akisisitza kuwa huenda akapata wazo hilo pale
ambapo Trump ataanza kutekeleza ahadi zake tata.
Micah
pia alithibitisha kutembelewa na maafisa hao wa usalama na kueleza kuwa
waliridhika na maelezo yake kuwa alikuwa anafanya utani tu, hivyo
waliondoka.
Trump
amekuwa akipata vitisho vya kushambuliwa tangu alipokuwa akiendesha
kampeni zake. Mara kadhaa maafisa usalama walimuondoa ghafla jukwaani
baada ya kuhisi jaribio la kutaka kumdhuru kutoka kwa wahudhuriaji.
Sign up here with your email