- Adama Barrow alizaliwa mwaka 1965 katika kijiji kimoja karibu na mji wa kibiashara wa Basse Mashariki mwa Gambia.
- Alihamia mjini London miaka ya 2000 ambapo anaripotiwa alifanya kazi kama mlinzi kwenye duka moja, Kaskazini mwa London, akiendelea pia na masomo yake.
- Alirejea nchini Gambia mwaka 2006 ambapo alianzisha kampuni yake ya kuwekeza.
- Barrow mwenye umri wa miaka 51 aliteuliwa kuongoza muungano wa vyama saba vya upinzani kumpinga Rais Yahya Jammeh.
- Amekosoa kutokuwepo kwa miula miwili kwa urais na pia kulaani kufungwa kwa wanasiasa wa upinzani.
- Anaunga mkono uhuru wa mahakama, wa vyombo vya habari na wa vyama vya umma.
Sign up here with your email