WANANCHI CHAMWINO WAANDAMAMNA KUDAI MAJI - Rhevan Media

WANANCHI CHAMWINO WAANDAMAMNA KUDAI MAJI

Tokeo la picha la MAJI FOLENI WAKAZI wa Kijiji cha Manzase wilayani Chamwino, wameandamana kijijini hapo kuibana Serikali iwapelekee maji.
Wananchi hao waliandamana juzi na kwenda katika ofisi za Serikali ya kijiji chao   kuonana na viongozi wao.
Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Emi Kaputi (47), alisema walilazimika kuchukua uamuzi huo kwa kuwa wamekuwa wakitembea umbali wa kilomita 10 kufuata maji katika Kijiji cha Mloda ambako pia wanauziwa   kwa Sh 500 kwa ndoo moja ya lita 20.
“Shida ya maji hapa kijijini kwetu imekuwa kubwa na imefikia hatua hata ndoa za watu zimeanza kuteteleka.
“Yaani tumefika mahali tumeanza kukata tamaa kwa sababu mara nyingi wanasiasa wamekuwa wakija hapa na kutupatia ahadi ambazo wanashindwa kuzitekeleza kuhusu haya maji,” alisema Kaputi.
Naye mwanafunzi wa Shule ya Msingi Manzase, Sarafina Julius (13), alisema tatizo la maji limesababisha  baadhi ya wanafunzi kushindwa kuhudhuria masomo  kutokana na kulazimika kuwasaidia wazazi wao kutafuta maji.
“Kule ni kilomita 10, kwa hiyo ukiangalia tunakwenda kilomita 20 kwenda na kurudi, hata hivyo tunashukuru kwa kuwa barabara ni nzuri vinginevyo hali ingekuwa mbaya zaidi,” alisema Sarafina.
Mhandisi wa Maji, Wilaya ya Chamwino, Grace Mukulasi, alikiri kuwapo   kero ya maji kijijini hapo akisema  tatizo hilo limesababishwa na uhaba wa fedha serikalini.
Diwani wa Kata ya Mlodaa, Peter Madanya (CCM), alisema uhaba wa maji kijijini hapo umekuwapo kwa miaka mingi.
Previous
Next Post »