Serikali
ya Mkoa wa Dar es Salaam imesema itawastaafisha kwa manufaa ya umma
watumishi wa mkoa huo walioshindwa kutekeleza majukumu yao kikamilifu.
Hayo
yalisemwa jana jijini humo na Mkuu wa Mkoa huo, Paul Makonda wakati
akizungumza na watumishi wa Manispaa ya Temeke akiwa katika ziara ya
siku mbili wilayani humo. Alisema watumishi wengi wamekuwa mizigo na
wanasubiri kuchukua mishahara bila kuifanyia kazi hivyo ni bora
kuwasimamisha kwa manufaa ya umma.
“Nafikiri
kuna haja ya kuwapunguza watumishi serikalini hakuna wanachofanya zaidi
ya majungu na umbea, asilimia 20 ndio wanaofanya kazi, tayari nimeongea
na Rais na kuna taratibu nakamilisha na tutachukua hatua,” alisema Makonda.
Aidha
Makonda alisema watumishi wengi wa umma wanaishia kula fedha za miradi
na matokeo yake wanatengeneza miradi mibovu ambayo imekuwa ikichukuwa
muda mfupi kuharibika.
Makonda
aliwashangaa watumishi wanaoshindwa kufanya kazi na kudai hawana bajeti
wakati wana uwezo wa kuzungumza na wadau na kupata fedha nyingi na
kuendesha miradi.
“Tumechoka
kusikia kelele za kukosa bajeti, yapo mambo hayahitaji bajeti lakini
hamfanyi tangu kuteuliwa kwangu nimeweza kufanya miradi ya zaidi ya Sh
bilioni 30 ambayo sio ya bajeti, lakini nyinyi mnapiga kelele za bajeti,
tukiona hamuwezi kubadilika tutawastafisha tunataka watu wanaofikiria
nje ya boksi,” alisema Makonda.
Sign up here with your email