WAKUU WA MIKOA SABA ' WAKALIA KUTI KAVU' - Rhevan Media

WAKUU WA MIKOA SABA ' WAKALIA KUTI KAVU'

Serikali imetoa muda wa hadi Januari mwakani kwa wakuu wa mikoa saba ambao mikoa yao haijamaliza tatizo la madawati kukamilisha kazi hiyo na kusema kwamba, iwapo watashindwa baada ya hapo watakuwa wameshindwa kwenda na kasi ya serikali ya awamu ya 5
Waziri wa TAMISEMI, George Simbachawene
Serikali imetoa muda wa hadi Januari mwakani kwa wakuu wa mikoa saba ambao mikoa yao haijamaliza tatizo la madawati kukamilisha kazi hiyo na kusema kwamba, iwapo watashindwa baada ya hapo watakuwa wameshindwa kwenda na kasi ya serikali ya awamu ya tano.
Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),  Mhe. George Simbachawene ametoa kauli hiyo leo Jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akipokea msaada wa madawati zaidi ya 3,500 kutoka Benki ya NMB ambayo yatatumiwa na wanafunzi wa shule za msingi na sekondari hapa nchini.
Mhe. Simbachawene amesema mikoa ambayo inaongoza kwa kuwa na hali mbaya ya ukosefu wa madawati na bado mpaka sasa wanafunzi wanakaa chini kuwa ni pamoja na mkoa wa Geita, Mwanza, Kigoma, Mara, Dodoma, Rukwa na Simiyu.
Previous
Next Post »