MBEYA CITY KUFUNGUA DIRISHA DOGO NOVEMBA 30 - Rhevan Media

MBEYA CITY KUFUNGUA DIRISHA DOGO NOVEMBA 30

Klabu ya Mbeya City imesema kwa sasa bado haijaanza zoezi la usajili kwani bado wanapitia ripoti ya kocha mkuu Kinnah Phiri ili kuweza kusajili wachezaji wenye viwango ambao wataipa timu hiyo manufaa.
Mbeya City

Afisa Habari wa Mbeya City Dismas Ten amesema,mara baada ya kufunguliwa kwa dirisha la usajili Novemba 15 mwaka huu kumekuwa na taarifa nyingi juu ya kuondoka kwa baadhi ya wachezaji wa timu hiyo kwenda kujiunga na timu nyingine pia  kusajiliwa kwa baadhi ya wachezaji kutoka timu nyingine kuingia ndani ya kikosi hicho suala ambalo mpaka sasa bado sio la kweli.
Ten amesema, taarifa zote kuhusiana na usajili mpya au kuachwa kwa wachezaji kwenye kikosi cha Mbeya City zitatolewa kuanzia Novemba 30 kwani kwa sasa uongozi bado unapitia na kufanyia kazi baadhi ya mambo muhimu yaliyopewa kipaumbele  kwenye ripoti ya mwalimu Phiri.
Previous
Next Post »