Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamiizi wa Mazingira Nchini,
NEMC limeipiga faini ya shilingi milioni kum na tano Halmashauri ya wilaya ya
Kahama kwa kile kinachodaiwa ni uzembe wa kuto zingatia sheria ya mazingira kwa
kuliweka Dampo la mji huo katika hali hatashi kwa mazingira na viumbe hai
wengine.
Katika Ziara ya Naibu Waziri Mpina Leo Mjini Kahama, ilohusisha
ukaguzi wa Dampo, machinjio viwanda na soko la mjini kahama kumebainika kuwa na
uzembe kwa watendaji wa Halmashauri ya mji wa Kahama, wa kutosimamia utupwaji
wa taka katika Dampo la mji huo ulohusisha kutupwa kiholela kwa taka ardhini na
kuteketezwa kwa njia isiyo salama.
Kufuatia ukiukwaji wa sheria ya mazingira ya 2004 na kanuni
zake, Baraza la mazingira nchini NEMC limeshawishika
kuitoza faini Halmashauri hiyo ya shilingi milioni kumi na tano na kutakiwa
kulipwa ndani ya wiki mbili.
Akiitaja adhabu hiyo mbele ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, Mkaguzi wa NEMC kanda ya ziwa na
Mikoa jirani Bw. Jamali Baruti sambamba na hilo ameleza kuwa, Halmashauri ya
Kahama inatakiwa kuboresha miondombi ya taka,kuratibu na kusimamia ujenzi wa
mabwawa katika machinjio mjini hapo kwani utupwaji holela wa samadi huchangia
uharibifu wa mazingira.
Akitilia msisitizo wa suala zima la uzingatiaji wa sheria ya
mazingira kwa watendaji nchini, Naibu Waziri Mpina alisema kuwa hawezi kukubali
kuwajibishwa sababu ya viongozi kushindwa kusimamia suala zima la mazingira, na
kuhaidi kuwawajibisha viongozi wazembe.
Awali, akitoa taarifa ta usafi wa mazingira ya wilaya ya Kahama
Mkuu wa Wilaya hiyo Bwana Nkulu alisema kuwa Kahama imekuwa ikikabiliwa na
chngamoto mbali mbali za kimazingira ikiwa ni Pamoja na uhaba wa magari ya
kuzolea taka, ukataji miti kwa matumizi ya kukaushia tumbaku, na usafishaji wa
dhahabu kwa kutumia madini ya zebaki ambayo si rafiki kwa mazingira.
Ziara ya Naibu Waziri
Mpina wilayani Kahama ni Muendelezo wa Ziara zake nchini za ukaguzi wa
mazingira na utekelezaji wa sheria ya mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake.
|