YANGA YAZIDI KUVURUGWA , AKILIMALI ATIMULIWA - Rhevan Media

YANGA YAZIDI KUVURUGWA , AKILIMALI ATIMULIWA

Ibrahim Akilimali, Katibu wa Baraza la Wazee wa klabu ya Yanga
Ibrahim Akilimali, Katibu wa Baraza la Wazee wa klabu ya Yanga

VIONGOZI wa Umoja wa Matawi wa Klabu ya Yanga umemsimamisha uanachama Ibrahim Akilimali, Katibu wa Baraza la Wazee wa klabu hiyo katika kikao cha dharula kilichofanyika Jangwani asubuhi ya leo, 
Akilimali amesimamishwa uanachama wa Yanga kwa kosa la kumdhalilisha mwenyekiti wa klabu hiyo kupitia kauli alizozitoa katika vyombo vya habari akipinga suala la mwenyekiti wa Yanga kukodishwa timu pamoja na nembo katika kipindi cha miaka 10.
Katika kikao hicho, Mzee Akilimali alikiri kumshambulia mwenyekiti wa klabu hiyo na kuwasilisha utetezi kuhusu kauli yake aliyoitoa katika vyombo vya habari juu ya suala hilo.
“Katika watu tunaompenda mwenyekiti, mimi namba moja lakini ikumbukwe mwana umleavyo ndivyo akuavyo, mwenyekiti alikuwa anatuita akitaka kufanya jambo ila siku hizi hatuiti wala hatuambii lolote anafanya tu.
Nimemwambia, mimi ndiyo nimempa uwenyekiti wa Yanga. Sisi tunampenda kweli, nilihoji kwa nia njema tu na nimemtaka radhi jana,” amesema.
Lakini Akilimali hakuishia hapo katika kutoa utetezi wake kuhusu kumtuhumu mwenyekiti pamoja na wanachama wa klabu hiyo kuwa, wamekurupuka katika kuamua vitu kwa haraka katika mkutano wa dharula wa klabu hiyo uliofanyika Diamond jubilee.
“Labda niseme hivi Kama kukurupuka ni tusi kama nilivyomwambia mwenyekiti, basi naomba radhi kwake Manji na wanayanga wote,” amesisitiza.
Pamoja na kutoa utetezi wake mbele ya kikao hicho, viongozi wa matawi wa klabu hiyo waliamua kumsimamisha uanachama kwa muda usiojulikana mzee Akilimali kwa kile kilichotajwa kama, kumkashifu na kumdhalilisha mwenyekiti wa klabu hiyo kongwe zaidi nchini.
Previous
Next Post »