Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva jana
alimtembelea Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Job
Ndugai nyumbani kwake Jijini Dar es Salam na kumjulia hali baada ya
kurejea kutoka nchini India alikokwenda kwa ajili ya matibabu.
Akiwa
nyumbani kwa spika Jaji Lubuva pia alimkabishi Mh. Ndugai ripoti ya
Uchaguzi Mkuu wa Rais Wabunge na Madiwani ya Mwaka 2015 na kumueleza
kuwa kukamilika kwa ripoti hiyo ndio hitimisho la Uchaguzi Mkuu na
maandalizi ya Uchaguzi Mkuu ujao.
Kwa
upande wake Mheshimiwa Ndugai aliipongeza hatua ya Tume ya Taifa ya
Uchaguzi ya kuweka mikakati ya kushiriki katika maonyesho mbalimbali
yakiwemo yale ya biashara SabaSaba na Nanenane katika kutoa elimu kwa
wananchi.
Jaji
Mstaafu Lubuva alikwenda kumjulia hali Ndugai ambaye kipindi cha Bunge
la Bajeti lililomalizika hivi karibuni, alikuwa nchini India kwa
matibabu na hivi sasa afya yake imezidi kuimarika.
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (kushoto)
akizungumza na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Job
Ndugai alipokwenda kumtembelea nyumbani kwake Salasala Jijini Dar es
Salaam.
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (kushoto)
akimkabidhi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Job
Ndugai ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka
2015 wakati alipokwenda kumtembelea nyumbani kwake Salasala Jijini Dar
es Salaam.
Sign up here with your email