MSEMAJI wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni,
Freeman Mbowe amesema jana kuwa wazo la Spika John Ndugai kutafuta
suluhu na wapinzani bungeni linakaribishwa, lakini akatoa angalizo
katika mkakati wa utekelezaji wake.
Akizungumza na kituo kimoja cha televishei cha jijini jana, Spika
Ndugai alisema itambidi aazime uzoefu kutoka kwenye bunge la katiba na
baadhi ya watu, wakiwamo maspika wastaafu ili kutafuta mwafaka wa
mvutano kati ya wabunge wa upinzani na Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson
uliojitokeza wakati wa bunge la bajeti.
Mbowe alisema upinzani unao tatizo katika kutumia maspika wastaafu
kwa sababu wote wanatoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) hivyo itakuwa ni
vigumu kutoa ushauri ambao utakuwa sawa kwa wote.
Alisema Spika Ndugai anapaswa kuwatumia pia wazee wastaafu kutoka
vyama vya upinzani wenye busara na hekima katika kutatua jambo hilo.
“Jambo moja la msingi ambalo kila mtu anapaswa kulitambua ni (kwamba)
hakuna mtu anayekataa ushauri bila ya kujali nani anatoa ushauri huo na
ni ushauri wa aina gani, lakini Spika anaweza kutafuta ama kuongeza
washauri kwa watu wengine nje ya CCM,” alisema Mbowe.
Mbowe alisema mara nyingi viongozi wa CCM linapokuja suala la utaifa
wanakuwa upande wa serikali, akitolea mfano mtafaruku uliotokea bungeni
mwaka jana kuhusu Katiba mpya.
Sign up here with your email