Baada ya lile sakata la NSSF kupiga chini zaidi ya wafanyakazi 200+ waliofoji vyeti, wiki hii TRA inatarajia kupiga chini watumishi wake zaidi ya 400 (437). Hawa ni walioingia bila sifa, waliofoji vyeti, walioingizwa na ndugu zao ambao waliokuwa vigogo...
Pamoja na hatua hiyo nzuri ila tunaomba serikali kuu isimamie hili zoezi kwa TRA, kwani kuna rushwa, na harufu ya kubebana ili kubakiza baadhi ya watumishi ambao hawana sifa...
Naomba nikuambie wazi kamishna Mkuu wa TRA, Ndugu Kidata ofisi ya HR inadhamiria kukudanganya katika hili zoezi. Wameamua kwa makusudi kulichukulia hili zoezi kimazoea. Hawajui hizi ni zama za Magufuli... Tafadhali Kamishna chukua hatua haraka sana.... Utadanganywa katika namba halisi...
Sign up here with your email