SAED
Kubenea Mbunge wa Jimbo la Ubungo jana alijisalimisha Kituo Kikuu cha
Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam na kuhojiwa kabla ya kupewa dhamana
kufuatia tuhuma za kuandika makala inayodaiwa kuwa ya uchochezi kuhusu
hali ya kisiasa Zanzibar.
Kubenea
ambaye anadaiwa kufanya uchochezi kwa kuandika makala katika gazeti la
MwanaHALISI toleo la 349 la Julai 25-31 yenye kichwa cha habari, ‘Yuko wapi atakayeiokoa Zanzibar?’
Kubenea
alifika katika kituo hicho cha Polisi jana saa saba na robo mchana
(13:15) akiwa na Tundu Lissu Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA) pamoja na Frederick Kihwelu wakili mwandamizi wa
Chama hicho.
Baaada
ya kuhojiwa kwa zaidi ya masaa mawili, saa tisa na robo alasiri (15:45)
alitoka na kuondoka huku wandishi wa habari wakishindwa kuzungumza naye
baada Jeshi la Polisi kuwazuia waandishi wa habari kuingia katika eneo
la kituo hicho.
Akizungumza
kwa njia ya simu, Lissu ambaye ndiye mwanasheria wa Kubenea katika
sakata hilo alisema kuwa, Kubenea amehojiwa kwa madai ya uchochezi
lakini alichokiandika ni hali halisi ya Zanzibar hususani visiwa vya
Pemba.
“Kubenea amechiwa kwa dhamana na ameamriwa kurudi tena kituoni hapo tarehe 18 Agosti, mwaka huu,” alisema Lissu.
Katika makala yake inayodaiwa kuwa ni ya kichochezi iliyokuwa na kichwa cha habari, “Yuko wapi atakayeiokoa Zanzibar?” Kubenea
alielezea jinsi Jeshi Polisi Visiwani Pemba wavyonadaiwa kuwabambikia
kesi wananchi, kuwapiga na kuwatesa kwa madai kuwa wananchi hao
wanaipinga serikali.
Kubenea
aliandika Makala hiyo baada ya kusafiri kutoka Dar es Salaam Mpaka
Zanzibar kufuatilia kile alichokitaja kama mateso, unyanyasaji na
ukiukwaji wa haki za binadamu dhidi ya wananchi wasio na hatia visiwani
humo.
Miongoni
mwa vijana na wahanga wa kubambikiwa kesi, kupigwa na kuteswa visiwani
Pemba waliotajwa na Kubenea katika makala yake ni ni Hijja Hassani
aliyetangazwa kuwa ni Mwakilishi wa Jimbo la Kiwani kabla ya Jecha Salim
Jecha Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kufuta uchaguzi.
Sign up here with your email