RAY C AVUNJA UKIMYA, AJA NA POST HIZI HAPA KUNAKO INSTAGRAM TOKA APELEKWE KWENYE MATIBABU BAGAMOYO - Rhevan Media

RAY C AVUNJA UKIMYA, AJA NA POST HIZI HAPA KUNAKO INSTAGRAM TOKA APELEKWE KWENYE MATIBABU BAGAMOYO

Ray C amepotea kwenye masikio na macho ya watu hivi karibuni baada ya tukio la kushangaza lililotokea June 16, 2016 maeneo ya Kinondoni ambapo Ray C alerikodiwa akipiga kelele kwenye gari ya polisi.
Ray C
Rehema Chalamila Aka Ray C alipelekwa Hospitali na polisi na baadae kwenda Rehab na baada ya hapo hatukusikia lolote kuhusu Ray C mpaka leo kwenye instagram yake..

Tafsiri ya maneno kwenye post ya kwanza >>
“Kupona huja kwanza, bili zitalipwa, kazi yako itaisha, mambo uliyopanda kufanya utafanya , kodi utalipa, familia yako itakupenda, upenda kwako utachanua zaidi , utapata ukipendacho, utafanya kinachotaka moyo, afya bora na utasimama na nguvu zaidi, ila Kupona huja kwanza".
Tafsiri ya maneno kwenye post ya pili>>
“Eh Mungu naomba amani ya kukubali yale nisiyoweza kubadilisha na hekima ya kujua utofauti, kuishi siku moja baada ya nyingine,kuwa na furaha muda wote ,nikubali kuna ugumu kwenye maisha, niwe na imani utafanya mambo yote yawe sawa kama nitakuwa na imani kwako, ili niwe na raha muda wote sababu yako".

Previous
Next Post »