Jeshi la Israel
linasema kuwa limeharibu nyumba ya raia wa Kipalestina aliyemdunga kisu
na kumuua msichana wa Iiisraeli chumbani mwake.
Jeshi hilo
limesema kuwa Mohammed Nasser Tarayrah alivunja na kuingia katika
nyumba iliopo katika makaazi ya Kiryat Arba mnamo mwezi Juni na
kumshambulia msichana huyo mwenye umri wa miaka 13 Hallel Yaff Ariel
alipokuwa akilala kabla ya kuuawa na mlinzi wa makaazi hayo.Sera ya Israel ya kuziharibu nyumba za raia wa Palestina wanaofanya mashambulio imekosolewa na wengi kama adhabu ya jumla.
Serikali ya Israel inasema kuwa hatua hiyo inawazuia wengine ambao wangependelea kutekeleza kitendo kama hicho.
Sign up here with your email