Ndege ndogo iliyokuwa na watu
sita imeanguka kwenye mti na kuteketea kwa moto wakati ikijaribu ikitua
Uwanja wa Ndege wa Shannon Kaskazini mwa Jimbo la Virginia nchini
Marekani, watu wote sita waliokuwemo kwenye ndege hiyo wameripotiwa
kufariki dunia jana Ijumaa.
Mashuhuda
wa tukio hilo waliokuwa wakisafii kwa treni wamesema walianza kuona
moshi na baadaye moto ukiwaka na waliposogea eneo la tukio waliona ndege
ndogo ikiwa imeanguka juu ya mti huku ikiteketea kwa moto. Aidha tarifa
zimeeleza pia kuwa hakuna mtu aliyeokolewa hata mmoja, wote waliokuwemo
wamefariki dunia.
Polisi katika Jimbo la Virginia wamesema
watu wote waliokufa siyo raia wa Marekani na kwamba miili ya marehemu
hao itapelekwa kwa Daktari Mkuu wa jimbo hilo, Richmond kwa uchunguzi
ili kuwatambua na kubaini ndugu zao.
Sign up here with your email