CHAMA cha chezo wa Pool Mkoa wa Dar es
Salaam kimeaandaa mashindano ya Pool katika
kusheherekea siku kuu ya nanenane
yatakayofanyika katika Viwanja vya TCC
Chang’ombe jijini Dar es Salaamyajulikanayo
kama “88” Pool Competitions 2016.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar
es Salaam, mratibu wa mashindano hayo,
Michael Machellah alisema maandalizi yako
vizuri kwani mpaka sasa mikoa 12
imeshathibitisha kushiriki ikiwakilishwa na
baadhi ya vilabu vyake.
Alisema Machellah mikoa hiyo ni pamoja na
Mkoa wa Dodoma,
Morogoro,Iringa,Mbeya,Pwani,Tanga,Kilimanjar
o,Arusha,Manyara,Mkoa wa kimichezo wa Ilala,
Mkoa wa kimichezo wa Kinondoni na Mkoa wa
kimichezo wa Temeke ambao ndio wenyeji wa
mashindano hayo.
Mashindano yao yanatarajiwa kuanza rasmi
Alhamis tarehe 4 Agosti 2016 na kumalizika siku
ya siku kuu ya nane nane tarehe 8 Agost 2016.
Zawadi katika mashindano hayo, Bingwa
upande wa timu ataibuka na Kashi shilingi laki
tano na kikombe, msindi wa pili 250,000/-,
mshindi wa tatu 150,000/- na mshindi wa nne
ni 50,000/-.
Upande wa mchezaji mmoja mmoja Bingwa
atazawadiwa Shilingi 200,000/-, wa pili shilingi
100,000/-, mshindi wa tatu 50,000/- na wan ne
ni shilingi 25,000/-.
Mwisho aliwaomba wadau na wapenzi wa
mchezo wa pool kujitokeza kuja kushuhudia
mashindano hayo katika Viwanja vya TCC
Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa mashindano ya Pool ya nane nane( “88” Pool Competition 2016), Michael Machellah (kushoto) akiwakabidhi Mwenyekiti wa Chama cha waamuzi wa mchezo huo, Hashim Sheweji(kulia) na Bingwa wa Afrika wa mchezo huo 2014, Patric Nyangusi, kikombe cha mshindi wa kwanza wa mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza kesho katika viwanja vya TCC Chang’ombe Mkoani Dar es Salaan.Picha Prona Momwi.
Sign up here with your email