MANECKY ASHANGAZWA NA BOB MANECKY KWA TUKIO HILI HAPA - Rhevan Media

MANECKY ASHANGAZWA NA BOB MANECKY KWA TUKIO HILI HAPA


Mmiliki wa A.M Records, Manecky amefunguka baada ya tetesi kuvuma kwamba amemuachia studio mdogo wake na yupo bize na maswala ya ndoa tuu.
Mmiliki wa A.M Records, Manecky
Week iliyopita Bob Manecky alihojiwa na eNEWZ kuhusiana na Manecky kuonekana mara chache kwenye studio hiyo, Na Bob Manecky akadai kuwa kwa sasa yeye ndio kama boss wa studio hiyo kwakuwa kaka yake huyo yupo busy na ndoa.
Akipiga story na eNEWZ, Manecky alijibu kwa kwakusema “studio ipo katika matengenezo na vitu kama hivyo maisha yanabadilika maisha huwezi kwenda bila kubadilika na maisha zamani nilikuwa naishi studio maisha yakabadilika kwa sasa nina familia so siwezi kwenda sehemu nikakaa bila kazi unataka kufanya kazi na mimi weka appointment tufanye kazi”.
Hata hivyo alisema Sababu ya Bob Maneke kuonekana pale studio ni kwasababu studio kuna vyumba pale pale na ndo sehemu wanapofanyia kazi “pale ndo maana unawakuta kila mara laikini kuna kipindi kitafikia watahama na kuendelea na maisha mengine” Aliseam Manecky.
Pia Manecky aliongezea kwakusema “Pia pale studio ni pahali ambapo ukifika mahali ukajiona kwamba unaweza kwenda unaweza ukahama kwa kuwa pale studio ni mahala pa kazi na nje kwa sasa wameweka fremu za biashara na wanakaa lakini wanalipa kodi pia”
Previous
Next Post »