TAMASHA la muziki la Fiesta 2016 limezidi kunogeshwa na wadhamini wakuu, Kampuni ya Simu ya Tigo, baada ya kutangaza msisimko wa kuwanufaisha wateja wake na mashabiki wa burudani katika tamasha hilo litakaloanzia Mwanza Agosti 20, mwaka huu.
Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga, alisema wamelenga kuwanufaisha wateja wao kwa kuwapatia vifurushi viwili vitakavyowawezesha kuchagua kati ya data za GB 1 au visivyo na ukomo vinavyojumuisha dakika 490 Tigo kwenda Tigo.
“Tamasha la Fiesta linawakaribisha Watanzania wote na pia tukio hilo linatoa shughuli za kijamii, tukiwa na kauli mbiu yetu Fiesta 2016 kwa Kishindo cha Tigo Imoooo,” alisema Mpinga.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa tamasha hilo, Sebastian Maganga, alisema tamasha hilo linaingia mwaka wa 15 likiandaliwa chini ya Prime Time Promotion na litajumuisha mikoa 15 ambayo ni Mwanza, Kahama, Kagera, Musoma, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma, Morogoro, Tanga, Kilimanjaro, Mtwara, Iringa, Mbeya na Dar es Salaam.
Sign up here with your email