Madiwani wa Ukawa wa Manispaa ya
Kinondoni wamesusa kikao kilichoitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Paul Makonda kwa madai kiongozi huyo hana uhusiano mzuri na
viongozi wa upinzani.
Jana, Makonda aliitisha kikao cha wakuu wa wilaya,
wakurugenzi, wakuu wa idara za manispaa za Temeke, Ilala na Kinondoni
na madiwani wote, wakiwamo wabunge wanaounda halmashauri hizo.
Kikao
hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Arnaoutoglou kililenga
kuzungumzia masuala mbalimbali, kama maeneo yaliyovamiwa na uboreshaji
wa elimu mkoani Dar es Salaam.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake, meya wa
Kinondoni, Boniface Jacob alisema Makonda amekuwa na tabia ya kudharau
na kutoheshimu viongozi wenzake, hasa wa upinzani akiwaona hawatendi
kazi vizuri.
Pia, Jacob alidai kuwa Makonda amekuwa na tabia ya
kuingilia kazi zinazofanywa na viongozi wengine kwa kutumia cheo cha
ukuu wa mkoa, jambo ambalo meya huyo alisema ni kinyume cha sheria.
“Akitaka tumpe ushirikiano, Makonda abadilike la sivyo mtindo utakuwa
huuhuu, mambo yatakuwa hivi. Huu ni mwanzo na ndiyo maana leo (jana)
Ukawa Kinondoni tumekuwa na msimamo mmoja,” alisema Jacob.
Jacob, ambaye
pia ni diwani wa Ubungo (Chadema), alisema hawakuona umuhimu wa kwenda
katika kikao hicho kwa sababu kiongozi wa mkutano huo anawadharau.
Akijibu tuhuma hizo, Makonda alisema madiwani waliohudhuria kikao hicho
maeneo yao yalikuwa na shida na yanahitaji kushughulikiwa, hivyo si kazi
yake kuhesabu watu na kubaini nani hakufika mkutanoni.
Alisema ajenda
kuu ya kikao hicho ilikuwa ni kujadiliana namna bora ya kuvirudisha
viwanja vilivyochukuliwa na kuvirejesha kwa matumizi yaliyokusudiwa.
“Huyo anayelalamika mwambie huo anaoufanya ni utoto akikua ataacha.
Narudia tena siyo kazi yangu kuangalia nani hajaja kwenye kikao,”
alisema.
Kwenye kikao hicho, meya wa Ilala (Chadema), Charles Kuyeko
alikuwapo kwenye mkutano huo pamoja na madiwani wenzake, sambamba na
wale wa Temeke.
Makonda si mgeni wa tuhuma .Aliteuliwa kuwa mkuu wa
wilaya ya Kionondoni katika kipindi ambacho alikuwa akituhumiwa kuhusika
kwenye sakata la kupigwa kwa Waziri Mkuu wa zamani, Jaji Joseph Warioba
kwenye mdahalo wa Katiba uliofanyika Hoteli ya Blue Pearl.
Katika
kipindi hicho, Makonda pia alikuwa akituhumiwa kumrushia tuhuma za
ufisadi Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa akiahidi kuwa CCM
isingempitisha kugombea urais.
Akitoa majumuhisho ya kikao cha jana
kilichoanza saa 2:00 asubuhi hadi saa 5:00 asubuhi, Makonda aliwataka
watu waliovamiwa na kujenga kwenye maeneo yasiyoruhusiwa, kuanza kubomoa
majengo yao kabla ya Serikali kuwafikia.
Kabla ya kutoa majumuisho hayo,
Makonda alitoa nafasi kwa madiwani wa manispaa hizo kueleza kero
zinazowakabili, hususan zinazohusu ardhi.
“Najua mchakato huu utawagusa
hadi vigogo, lakini mimi siogopi vita kwa sababu ndani yangu ninaongozwa
na Mungu pekee,” alisema Makonda.
Mbali na hilo, Makonda
alisema endapo mtendaji wa ardhi atayebainika kuhusika katika kuchezea
michoro na ramani ili aachie ardhi na kujipatia fedha, atashughulikiwa
kwa mujibu sheria.
Katika hatua nyingine, Makonda amemwagiza kamishna
msaidizi wa ardhi wa Kanda ya Dar es Salaam, Mathew Nhange kumwambia
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi awaondoe
maofisa ardhi na mipango miji wa Kinondoni na Ilala baada ya kushindwa
kutoa taarifa za kuridhisha katika mkutano huo.
Huku akiwataja maofisa
hao wanaotoka Kinondoni na Ilala, Makonda alisema alishakutana na wakuu
wa idara kwenye vikao vilivyopita, hivyo alitegemea kuwa watumishi hao
wangetoa taarifa zilizokamilika.
“Kamishna naomba umwambie katibu mkuu
mimi siwataki watumishi hawa katika manispaa hizi. Mwambie awatoe na
kuwapangia kazi nyingine,” alisema Makonda.
Kamishna Nhange alisema agizo hilo analifanyia kazi na kwamba atampa katibu mkuu taarifa za watumishi hao jana.
Kamishna Nhange alisema agizo hilo analifanyia kazi na kwamba atampa katibu mkuu taarifa za watumishi hao jana.
Sign up here with your email