Takataka zilizotelekezwa eneo la Kimara, Korogwe-Jeshini na kuwa kero kwa wakazi wa eneo hilo.
WAKAZI wa mtaa wa Kimara, Korogwe-Jeshini uliopo ndani ya Manispaa ya Kinondoni wapo hatarini kupata magonjwa ya mlipuko kutokana na uchafu mwingi uliotelekezwa na wahusika wenye jukumu la kuzoa uchafu eneo hilo.
Kwa mujibu wa wakazi wa eneo hilo, ni kwamba takataka hizo zimetelekezwa hapo wiki zaidi ya tatu zilizopita hali iliyozua usumbufu na kero kwa majirani na wapita njia wa eneo hilo.
“Tunaomba serikali itusaidie kumkemea wakala aliyeshika tenda ya kuzoa takataka kwenye eneo hili kwa sababu ametelekeza uchafu hapa na zaidi ya wiki tatu gari la taka halijaja fikiria mvua ikinyesha hapa itakuwaje.” Alisisitiza mwanamke mmoja mkazi wa jirani wa eneo hilo ambaye hakuwa tayari jina lake kuwekwa mtandaoni.
Sign up here with your email