CHRISTIAN BELLA : AOMBA KUKUTANA NA RAIS JPM - Rhevan Media

CHRISTIAN BELLA : AOMBA KUKUTANA NA RAIS JPM


Christian Bella & Malaika Band - AmerudiChristian Bella.
Na Leonard Msigwa
MWANAMUZIKI Christian Bella maarufu kwa jina la ‘King of Best Melody’ amefunguka na kuweka wazi dhamira yake ya kuomba kuonana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dk. John Pombe Magufuli, Ikulu jijini Dar es Saalam bila kuweka wazi lengo maalum la kusudio hilo.

JIPU RAIS-MAGUFULI-6
Rais Dk. John Pombe Magufuli.
Mwanamuziki huyo anayefanya vyema nchini kwa sasa akitamba na wimbo mpya wa Nishike, ametamka hayo baada ya kufanya ‘Show’ mbele ya Rais Magufuli kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara jijini mwanza wiki iliyopita.

Akizungumzia ‘show’ hiyo Bella amesema, “Nilistushwa na waandaaji wa mkutano wa mheshimiwa rais kwamba nimeteuliwa kwenda kuimba mbele ya mheshimiwa rais, nilifurahi kupata nafasi hiyo adimu, siku ya tukio nilipanda jukwaani na kuimba vizuri wimbo wa Usilie huku nikichomekea maneno, “wanyonge wasilie kimbilio na mwokozi wao ni Rais Magufuli”, baada ya ‘show’ nilienda kumpa mkono na sikufanya makosa hapo hapo nikamdokeza kusudio langu la kuomba kuonana naye.

“Pia wakati nikimpa mkono mheshimiwa rais alisema anazipenda sana nyimbo zangu na nilifurahi sana kusikia kauli hiyo kutoka kwa kiongozi mkuu wa nchi na naahidi nitaendelea kutoa nyimbo kali zaidi” Alisisitiza Bella.
Previous
Next Post »