Shirikisho
la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), leo saa 6:00 usiku litafunga
tena dirisha la usajili baada ya kulifungua jana kwa saa 48 na
imebainika kuwa timu tatu zaidi zilikuwa na dosari katika usajili hivyo
kufanya ongezeko la kutoka timu nane zilionekana kwa haraka mapema wiki
hii mara baada ya dirisha kufungwa Agosti 6, 2016.
Timu
hizo kwa ujumla zilikuwa na dosari ya ama kutokusajili kabisa au
kutokamilisha usajili wa ushiriki wa ndani kwa msimu wa 2016/2-17. Timu
tatu nyingine zilizobainika leo Agosti 14, 2016 katika mtandao ni pamoja
na Toto African ya Mwanza na Stand United ya Ligi Kuu Tanzania Bara
kadhalika Arusha FC ya Arusha ambayo msimu huu itashiriki Ligi Daraja la
Pili (SDL).
Hadi
tunatuma taarifa hii usajili ulikuwa ukiendelea kwa mfumo wa mtandao
(TMS) ikiwa na maana ya Transfer Matching System, lakini Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limerejea kanuni za usajili hivyo
kuzitoza faini timu zilizokuwa na dosari. Faini imetozwa kwa viwango
tofauti kulingana na mashindano.
Timu
zinazohusika na usajili wa mtandao ni zile zinazoshiriki Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara (VPL), Ligi Daraja la Kwanza la StarTimes (SFDL)
na Ligi Daraja la Pili (SDL) na adhabu ya kushuka daraja na kwenda
kushiriki Ligi ya Wilaya kisha Ligi ya Mabingwa Mikoa (RCL) ambayo
usajili wake ni wa kutumia karatasi.
Timu
za Ligi Kuu ambazo zilikatiwa mawasiliano baada ya kushindwa kuwahi
tarehe ya mwisho ya usajili ni Young Africans ambayo haikusajili kabisa.
Kwa kufanya makosa hayo, kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu ya Vodacom,
Young Africans imeadhibiwa faini ya shilingi milioni tatu (Sh.
3,000,0000). Young Africans imetozwa faini hiyo kwa kutosajili jina hata
moja kabla ya Agosti 6, 2016.
Timu
nyingine za Ligi Kuu ambazo hazikukamilisha usajili angalau kufikisha
wachezaji 18 ni African Lyon ya Dar es Salaam, Stand United ya Shinyanga
na Toto African ya Mwanza ambazo kila timu imetozwa faini ya shilingi
milioni moja (Sh.1,000,000).
Kwa
timu za Daraja la Kwanza la StarTimes (SFDL), Coastal Union ya Tanga
pekee imetozwa faini ya shilingi milioni moja (Sh.1,000,000) wakati timu
nyingine za daraja hilo, Kiluvya United na Friends Rangers za Dar es
Salaam pamoja nna Panone, zimetoswa faini ya shilingi laki tano (Sh.
500,000) kila moja.
Kadhalika
kwa timu za Daraja la Pili (SDL), ambazo ni Kitayose ya Kilimanjaro,
Mashujaa ya Kigoma na Arusha FC ya Arusha, zimetozwa faini ya shilingi
laki tano (Sh. 300,000) kila moja. Faini hiyo ni kwa timu na uongozi
husika hauna budi kuilipa mara moja, kwani TFF haitatoa leseni za
wachezaji kama timu haijalipwa faini hiyo.
Kanuni
zinazozungumzia usajili ni Sura ya 10 inayozungumzia usajili na 11
inayozungumzia Adhabu Zihusuzo Usajili Na Uhamisho kadhalika Uhamisho
Nje ya Nchi.
Sign up here with your email