Mnara
wa wa ‘Eiffel Tower’ uliopo jiji la Paris nchini Ufaransa unakadiriwa
na thamani mara sita zaidi ya ule wa Colloseum uliopo Rome wenye thamani
ya euro bilioni 91 (paundi bilioni 72) ambao ndiyo unafutia kwa karibu.
Mnara
huu siku ya leo ni kama siku yake ya kuzaliwa kwani siku Agosti 14,
wajengaji walikamilisha sehemu ya pili ya gorofa ya pili ya mnara huo
wenye thamani kubwa zaidi uliojengwa mwaka 1888.
Hata
hivyo mnara huu utabaiki kuwa wa thamani na kivuti zaidi kwa watu wengi
wanaotembelea jiji hilo lenye kila aina ya raha na starehe.
Majibu
ya tafiti zilizofanywa na Taasisi za Kibiashara za Monza na Brianza za
nchini Italy juu ya uzuri wa muonekano na umaarufu ulitokana na
kuangalia vigezo vyote kati ya minara 10 tofauti iliyofanyiwa uchambuzi
na takwimu za kina na mashirika mbalimbali
Kigezo
kilichozingatiwa ni pamoja na kielelezo cha wingi wa watalii, thamani
ya kiuchumi kwenye eneo husika, umaarufu wa mnara husika, wingi wa ujio
wa wageni kwenye mnara au eneo husika na vile vile namna unavyovutia
kiuchumi, kwa vigezo kama vile idadi ya ajira zinazotengenezwa. Mnara wa
huu wa Eiffel unakadiriwa kuwa na urefu wa futi 1,050, unashika nafasi
ya tano kwa kuingiza pato la taifa nchini Ufaransa.
Mwandishi wa mtandao huu Andrew Chale, akiwa katika moja ya eneo la mnara huo wa Paris, juu kabisa ya kilele cha mnara huo.
Mwandishi
wa mtandao huu Andrew Chale, akiwa katika moja ya eneo la mnara huo wa
Paris, juu kabisa ya kilele cha mnara huo. Hapa akiangalia taswira ya
mbali
Mwandishi
wa mtandao huu Andrew Chale, akiwa katika moja ya mitaa ya Paris jirani
kabisa ya mnara huo.uzuri ukiwa Paris mnara huu unaweza kuonekana
mahala popote pale…
Mwandishi
wa mtandao huu Andrew Chale,akiwa jirani na mnara huo majira ya jioni.
Mnara huu wa Eiffel tower unakuwa na tabia ya kubadirika rangi kipindi
cha usiku kwa kuvutia taa za kila aina. Hakika unavutia sana. (Picha
zote na Modewjiblog team).
Sign up here with your email