Ndege ya Shirika la Ndege la Emirates
iliyokuwa ikijiandaa kutua katika Uwanja wa Kimataifa wa Dubai imewaka
moto na kusababisha taharuki kubwa kwa abiria waliokuwamo kwenye ndege
hiyo.
Ndege
hiyo Boeing 777-300 ilikuwa na abiria 282 na wafanyakazi 18 na hakuna
aliyejeruhiwa. Abiria wote waliokolewa kupitia mlango wa dharura wa
ndege hiyo iliyouwa ikiruka kutoka Trivandrum, India.
Waliondolewa
kwenye eneo la tukio ndani ya dakika 45 tangu kwa ndege hiyo kuwaka
moto huku vyombo vya zimamoto zikichukua hatua ya haraka kuudhibiti moto
huo.
Ndege
hiyo iliwaka moto muda mfupi baada ya kutua kwenye uwanja huo na kwamba
hadi sasa hakuna taarifa za kile kilichobabisha kuzuka kwa moto huo.
Miongoni mwa
abiria waliokuwemo kwenye ndege hiyo ni pamoja na 24 Wabritons, sita
Wamarekani, wanne Waireland na wawili Waustralia.
Sign up here with your email