AGIZO LA RAIS MAGUFULI LATEKELEZWA , STEND YAANZA KUTUMIKA BAADA YA MIAKA 10 - Rhevan Media

AGIZO LA RAIS MAGUFULI LATEKELEZWA , STEND YAANZA KUTUMIKA BAADA YA MIAKA 10

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli wakati wa ziara yake mkoani Tabora alitoa maagizo kadhaa kwa watendaji likiwemo agizo la kufunguliwa kwa stendi ya mabasi Igunga ambayo ilikamilika na kuacha kutumiwa kwa miaka 10.

Rais aliwapa siku mbili watendaji wa mkoa na SUMATRA wahakikishe stendi inaanza kutumia kuanzia Juzi Jumatatu.

Kufuatia agizo hilo tayari SUMATRA kwa kushirikiana na jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani wameanza kuelekeza agizo hilo na magari yote ya abiria yanayopita Tabora yameanza kupita katika stendi hiyo.

Akizungumza wakati wa kukagua utekelezaji wa agizo hilo Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amesema SUMATRA washirikiane na jeshi la polisi kuhakikisha kila gari la abiria linapita na dereva atakayekaidi agizo hilo anyang'anywe leseni.

Kwa upande wao, wananchi wamepongeza sana uamuzi wa Rais huku wengine wakiulalamikia uongozi wa wilaya kwa kulea tatizo kwa muda wa miaka 10 wakati utatuzi haukuchukua siku tatu.
Previous
Next Post »