KAUZU YATINGA NUSU FAINALI MICHUANO YA NDONDO CUP, SASA KUKIPIGA NA MISOSI - Rhevan Media

KAUZU YATINGA NUSU FAINALI MICHUANO YA NDONDO CUP, SASA KUKIPIGA NA MISOSI





Timu ya Kauzu Fc imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali michuano ya Ndondo Cup, baada ya kuifunga Kibada Fc bao 1-0 katika mchezo wa robo Fainali iliopigwa jana jioni kwenye Uwanja wa Bandari, jijini Dar es Salaam.

Bao hilo pekee lilifungwa na Rashidi Roshwa, katika dakika za lala salama.

Akizungumza na mtandao huu baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Kocha wa Kauzu Fc Mashaka Said, alisema kuwa wamefurahia matokeo hayo na kutinga Nusu fainali mwaka huu ba kusema kuwa wanajipanga na maandalizi ya kutosha ili waweze kuchukua hasa baada ya mwaka jana kufungwa na waliokuwa mabingwa Faru Jeuri.

Kwa hatua hiyo Kauzu wanaungana na timu za Temeke Market, Makumba Fc pamoja na Misosi katika hatua ya nusu fainali inayotarajia kuwa mwishoni.mwa wiki ijayo huku Kauzu wakitarajiwa kuvaana na Misosi kwenye hatua hiyo.

Katika michuano hiyo ya Ndondo Cup kumekuwa na matukio mengi na ya kila aina huku pia ikisheheni wachezaji wengi wa Ligi Kuu wanaozichezea timu zao za mitaani, ambapo katika mchezo wa leo uliokuwa mkali na kusisimua uliweza kuwavutia mashabiki wengi wa soka waliopata burudani murua kutoka kwa baadhi ya wachezaji wa Ligi kuu.

Kikosi cha Kibada FC

Kikosi cha Kauzu FC


Vimbwanga vya mashabiki

Mtaalam wa Kibada FC akiingia uwanjani na kamati yake ya Ufundi

Mtaalam wa Kauzu FC akiwa kabebwa juu juu wakati akiletwa uwanjani kufanya mambo ili timu yake ishinde.

Previous
Next Post »