AIBUKA KIKAO CHA RC KUDAI FIDIA - Rhevan Media

AIBUKA KIKAO CHA RC KUDAI FIDIA



Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla



Mbeya. Mkazi wa Jiji la Dar es Salaam, Gibson Mwasembo ameibuka kwenye kikao cha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akitaka kulipwa fidia kwa madai ya kugongwa na gari la mkuu wa mkoa huo mwaka 1980 na kupata ulemavu.

Jana, Makalla alihamishia ofisi yake katika Ukumbi wa Benjamini Mkapa kwa lengo la kusikiliza kero na matatizo ya wananchi.

Hata hivyo, Makalla aliwataka watendaji wa ofisi yake kuwasiliana na mzee huyo ili hatua zaidi za suala lake lifanyiwe kazi.

Previous
Next Post »