Wanasayansi nchini
Marekani wanajaribu kukuza viungo vya binadamu ndani ya mwili wa
nguruwe, wakitumia teknolojia mpya inayofahamika kama 'Gene Editing'.
Wanasayansi
hao wametoa vinasaba vinavyosaidia ukuaji wa kongosho kwenye nguruwe na
badala yake wanaweka chembe chembe za viungo vya binadamu kwa matarajio
kuwa kongosho ya binadamu itakua.Hata hivyo teknolojia hiyo mpya inapingwa vikali na wanasayansi wengine kwa sababu ya maadili ya udaktari.
Wanasayansi hao wanadai kuwa huenda chembe chembe za binadamu zitakuwa na kufika kwenye ubongo wa nguruwe unaoendelea kukuwa.
Sign up here with your email
