PARIS, Ufaransa
TIMU ya taifa ya Ufaransa
inafungua pazia la michuano ya Euro 2016 leo Ijumaa katika mtanange
dhidi ya Romania huku ikiwa inapewa nafasi kubwa zaidi ya kutwaa ubingwa
wa mwaka huu. Mechi ya leo itaanza majira ya saa 4:00 usiku kwa saa za
Afrika Mashariki. Timu nyingine zilizopo kwenye kundi moja na Ufaransa,
ukiachana na Romania, ni Albania na Uswisi.
Romania wanaonekana kuhangaika katika
kufunga mabao lakini ukuta wao ni mgumu kupitika. Hatari kubwa ya
Ufaransa ni katika ulinzi baada ya Raphael Varane na Lassana Diarra kuwa
majeruhi. Laurent Koscielny na Adil Rami, wanaonekana ndiyo
watakaochezeshwa leo katika ukuta wa kati lakini ni mara chache
wamecheza pamoja na walipocheza walionyesha kutokujiamini na makosa
kibao.
Sign up here with your email
